Wamiliki wa silaha mkoani Manyara watakiwa kuhakiki silaha zao
24 July 2024, 4:06 pm
Kamanda wa wa polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na timu kutoka makao makuu ya polisi Dodoma watafanya uhakiki wa silaa kwa wamiliki wa silaa ili kujiridhisha kama anuani ya mmiliki wa silaa imebadilika na kujiridhisha kama wamiliki wa silaa bado wapo hai na alama zinazo itambulisha silaa.
Na. Angela Munuo
Jeshi la polisi mkoani Manyara limewataka wamiliki wa silaha mkoani hapa kujitokeza katika vituo vya polisi ili kuhakiki silaha wanazomiliki na kuhuisha taarifa za wamiliki wa silaha kisheria.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara George Katabazi ameyasema hayo julay 23 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na timu kutoka makao makuu ya polisi Dodoma watafanya uhakiki wa silaa kwa wamiliki wa silaa ili kujiridhisha kama anuani ya mmiliki wa silaa imebadilika na kujiridhisha kama wamiliki wa silaa bado wapo hai na alama zinazo itambulisha silaa .
Aidha kamanda Katabazi amewataka wamiliki wa silaha kuwa makini na silaa wanazotumia kutobeba silaa wakiwa wamelewa au kuiacha katika mazingira yasiyo sahihi kwakua inaweza kuleta taharuki katika jamii au kuchukuliwa na watu wenye nia ovu na kufanya uhalifu.