Wafanyabiashara 8 wanaotumia vipimo batili wakamatwa Manyara
22 July 2024, 5:24 pm
Msako wa kuondoa vipimo batili kwa wafanyabiashara ambao wamekaidi agizo la kutumia mizani kupimia bidhaa mbali mbali katika masoko ya mji wa Babati mkoani Manyara unaendelea kwa kuwafikisha katika kituo cha polisi.
Wakala wa vipimo mkoani Manyara kwakushirikiana na jeshi la polisi wamefanya msakoya kuondoa vipimo batili katika masoko ya mji wa Babati ambapo wafanyabiashara 8 wa wanaofanya biashara ya mazao mbali mbali katika masoko hayo wamekamatwa na kulipishwa faini.
Akizungumza na fm Manyara meneja wa wakala wa vipimo mkoani Manyara Denis Misango amesema oparesheni hiyo imeanza julay 18 2024 kwa kutoa elimu kuhusu matumizi ya mizani kupimia bidhaa zao na kuachana na vipimo batili kama makopo na madebe .
Aidha Misango amesema oparesheni hiyo ya kuondoa vipimo batili kwa wafanyabiashara wote inaendelea ambapo amewataka wafanyabiashara wote mkoani Manyara ambao wanaendelea kutumia vipimo batili kuacha mara moja kwakua ni kinyume na sheria .