BoT yazitaka taasisi za kifedha Manyara kujisajili
28 June 2024, 5:15 pm
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutokuchukua mikopo kwa wakopeshaji binafsi ili kuondokana na riba kandamizi pamoja na kujua sheria itakayo mlinda pindi anapochukua mkopo katika Taasisi za kifedha
Na Emmy Peter
Tasisi za huduma ndogo za fedha zinazokopesha fedha wilayani Babati mkoa wa Manyara zimetakiwa kujisajili Bank kuu ya Tanzania BOT ili kupatiwa lesseni za biashara katika hutoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi .
Akizungumza katika kikao cha wafanya biashara watoa huduma ndogo za fedha kilichofanyaka june 27 2024 katka ukumbi wa White rose wilayani Babati mkoani Manyara, Meneja msaidizi wa huduma ndogo za fedha kutoka makao makuu ya Bank kuu ya Tanzania BOT Dar es salaam Mary Ngassa amesema wanatoa elimu kwa wakopeshaji ili wafahamu sheria za ukopeshaji fedha kwa wananchii
Kwa upande wake Afisa biashara mkoa wa Manyara Fue Chedieli amesema kila mkopeshaji fedha anatakiwa kuwa na lesseni daraja “A” na amewataka wananchi kutokuchukua mikopo kwa wakopeshaji binafsi ili kuondokana na riba kandamizi.
na amewataka kujua sheria itakayo walinda
Aidha watoa huduma ndogo za kifedha wilayani Babati mkoani Manyara wameishukuru Bank kuu ya Tanzania BOT kwa kuwapa elimu hiyo kwakua awali hawakuwa wanajua nakusema itawasaidia wakopeshaji ambao hawafahamu sheria za ukopeshaji.