FM Manyara

Vituo vya mafuta Manyara fuateni bei elekezi ya petrol na dizel

June 5, 2024, 11:53 pm

Picha ya pampu ya mafuta

Baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) kanda ya kaskazini kutangaza bei mpya za mafuta ya dizel na petrol  wafanyabiashara na wananchi mkoani hapa wametakiwa kufuata utaratibu wa bei hiyo

Sauti Hawa Rashid

Wafanyabiashara vituo vya mafuta ya dizel na petrol  mkoani Manyara wametakiwa kufuata utaratibu wa bei elekezi zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya kaskazini ambazo ni bei kikomo.

Meneja wakanda ya kaskazini Mhandisi Lorivii Long’idu ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Fm Manyara, amesema bei mpya za mafuta ya petrol na dizel kwa kanda ya kaskazi zimeanza kutumia rasmi leo june 5 na zitadumu kwa mwezi mzima ambapo amewataka wafanyabiashara kufuata bei hizo elekezi na wananchi  kununua mafuta kutokana na bei iliyowekwa.

Sauti ya Mhandisi Lorivii Long’idu

 Mhandisi Lorivii amesema  bei hizo zimekuwa na mabadiliko ikilinganishwa na bei za mwezi may uliopita na kupungua kwake kumechangiwa na bei za ununuzi katika soko la dunia ambapo mafuta yalipungua kwa asilimia 11.82 kwa mafuta ya petroli na asilimia 7.77 kwa mafuta ya dizel na asilimia 7.94 kwa mafuta ya taa.

Aidha,amesema kwa kanda ya kaskazini wanachukua mafuta katika Bandari ya Tanga ambazo bei zimepungua na upungufu huo umetokana na kupungua kwa ghara katika soko la dunia na unafuu unaonekana katika soko la ndani.

Sauti ya Mhandisi Lorivii Long’idu