Wazazi watakiwa kusimamia ndoto za watoto wao
4 June 2024, 6:36 pm
Katika kipindi hiki cha likizo kumekuwa na tabia ya wazazi kuwapa watoto kazi nyingi za nyumbani hali inayopelekea watoto kusahau walichofundishwa shule nakushindwa kutimiza ndoto zao
Na Marino Kawishe.
Wazazi na walezi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kuwasisimamia watoto wao katika kipindi hiki cha likizo ili wajisome badala ya kuwatumikisha na shughuli za nyumbani
Wito huo umetolewa na Afisa elimu msingi Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani hapa Getrude Kavishe alipokuwa akiongea na Fm Manyara, amesema katika kipindi hiki cha likizo kumekuwa na tabia ya wazazi kuwapa watoto kazi nyingi za nyumbani hali inayopelekea watoto kusahau walichofundishwa shule.
kwa upande wake Afisa elimu kata ya endakiso Milikiori Gobre amesema wamekuwa wakiweka muda waziada kwa kwatoto kujisomea ili kuendelea kukuza uelewa wao ambapo amewataka wazazi kuwapa nafasi watoto wao katika masomo ikiwemo kuonyesha ubunifu na kuwapa muda wa kujifunza kufanya shughuli mbali mbali za kiubunifu .
Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo amewataka watoto kuzingatia wanayofundishwa ili kutimiza ndoto zao kwakua zinaanzia utotoni hadi kufikia malengo yao ikiwemo kuwa marubani na madakta.