Mashine 49 za mchezo wa kubahatisha zakamatwa Manyara
3 June 2024, 5:15 pm
Kamanda wa polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi awataka wamiliki na wafanya biashara wa michezo ya kubatisha kuzingatia taratibu za sheria na kanuni zilizowekwa na bodi ya michezo
Na Emmy Peter
Jeshi la polisi mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na maafisa kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini wamekamata mshine 49 maarufu kwa jina la Dubwi ambazo zilikuwa zikifanya kazi kinyume na sheria bila kuwa na leseni na kukwepa kulipa kodi ya serikali
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani mkoani Manyara George katabazi Amesema watuhumiwa watano wamekamatwa na jeshi hilo pamoja na mshine sita ambazo zilikuwa zikimilikiwa na watu wawili bila kufuata sheria za kumiliki mshine hizo za mchezo wa kubatisha.
Aidha kamanda Katabazi amewataka wamiliki na wafanya biashara wa michezo ya kubahatisha kuzingatia taratibu za ,sheria na kanuni zilizowekwa na bodi ya michezo ikiwa ni pamoja na leseni na kuchangia pato la serikali pamoja na miongozo iliyowekwa kwa wamiliki hao.