FM Manyara

Silo atoa magunia 10 ya mahindi kwa waathirika Manyara

May 22, 2024, 7:10 am

Picha ikiwaonyesha viongozi wa Babati vijijini

Wakazi  500  katika kata  Magara  wilayani Babati  mkoai Manyara  wamekosa mahali pa kuishi baada ya  nyumba  zao  kufunikwa na maji ya ziwa Manyara kutokana na ziwa hilo  kufurika  kutokana na   mvua.

Na Emmy Peter

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Babati Vijijini Danieli Silo  ametoa magunia 10 ya mahindi  kwa  zaidi ya wakazi 500  kutoka kaya 311 katika kata  Magara  wilayani Babati  mkoani Manyara  ambao  nyumba  zao  zimefunikwa na maji ya ziwa Manyara kutokana na ziwa hilo kufurika  kufuatia  mvua zinazoendelea kunyesha nchini. 

Akiongea na FM Manyara Silo amesema alifika  katika eneo hilo akiambatana na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Babati Vijijini akiwemo mkurugenzi Anna Mbogo pamoja na Wakuu wa Idara ili kujionea hali halisi na kufanya tathmini ya athari iliyotokea  kwa wakazi ambao wamekosa makazi ya kuishi kwa kuwapelekea  mahema pamoja  na chakula.

Aidha Silo amesema hakuna madhara yoyote yaliyojitokeza  kwa wakazi hao  zaidi ya  mazao ya chakula kyalichokuwa katika mashamba ambayo hayajavunwa  na kuwataka kuendelea kuchukua tahadhari ya maji hayo na kama walivyotangaziwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania  (TMA) kuhusu mvua zinazoendele kunyesha .

Sauti ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na mbunge wa Babati vijijini

Kwa upande wake mkurugenzi wa Babati vijijini Anna Mbogo  amewapa pole wakazi hao nakusema Halmashauri  inafanya utaratibu kwa ambao wamekosa mahala pakuishi na kama kunagarama zozote watagharamia.

Sauti ya mkurugenzi wa Babati Vijijini