Pelekeni watoto wa kike shule Manyara
20 May 2024, 11:53 am
Jamii za kifugaji mkoani Manyara zimekiwa kucha tabia ya kumuozesha mtoto wa kike na badala yake kumpa elimu ambayo itamsadia kwakua anamchango mkubwa katika jamii.
Na Angela Munuo
Wazazi na walezi wa jamii ya kimasai wilayani Simanjiro mkoani Manyara wametakiwa kuona umuhimu kuwapatia elimu watoto wa kike kwakua binti anapofanikiwa kupata kazi anamsaada mkubwa kwa familia na jamii kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika chuo cha wanawake na vijana cha Icrate Foundation katika kijiji cha endoret wilayani Simanjiro mkoani Manyara,ambapo amewataka wazazi kuachana na tabia ya kuwaozesha watoto wakike na badala yake kuwaacha wapate elimu.
kwa upande wa wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbali mbali wanaosoma kwenye chuo hicho wamelishukuru shirika la Icrate foundation kwa kufanikisha mradi huo ambo utawasaidia watoto wa kike kujikukwamua kiuchumi kutokana na mafunzo wanayoyapata ya ujasiriamali yanayofundishwa chuoni hapo.