Wananchi Manyara wekezeni TIC
20 May 2024, 10:04 am
Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki ili kuvutia wawekezaji ambao wanaongeza thamani katika mazao yanayolimwa na wakulima mbali mbali hapa nchini ambapo watanzania wametakiwa kutumia fursa hizo ili kusajili miradi yao na TIC.
Na George Agustino
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutumia fursa ya uwekezaji inayotolewa na kituo cha uwekezaji Tanzania TIC kwa kuwekeza miradi mbali mbali katika sekta ya viwanda, sekta ya kilimo, sekta ya afya, sekta ya usafirishaji, sekta mawasiliano pamoja na sekta ya utali ambazo zina mchango mkubwa kwa jamii.
Hayo yamesemwa na kaimu meneja wa kituo cha uwekezaji kanda ya kaskazini Veronica Tadeus alipokuwa akiongea na Fm Manyara, amesema miongoni mwa sekta zinazokuwa kwa kasi zaidi ni nchini ni sekta ya utalii, kilimo pamoja na sekta ya viwanda ambapo amewataka watanzania kuchangamkia fursa hizo zinazotolewa na kituo hicho hasa katika kanda ya kaskazini kwa lengo la kuzalisha ajira kwa wingi.
Vero amesema mkoa wa manyara unafursa nyingi katika kilimo na ardhi yake ina rutuba ya kutosha katika kilimo cha ngano na alizeti ambapo amewataka watanzania kutumia fursa hizo kwa kusajili miradi yao na TIC kwakua watapata vivutio mbali mbali vya kikodi.
Aidha amesema kwa kanda ya kaskazi kituo cha uwekezaji Tanzania TIC kinahudumia mikoa minne ikiwemo mkoa wa Manyara,Arusha,Tanga na Kilimanjaro,na serekali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki ili kuvutia wawekezaji ambao wanaongeza thamani katika mazao yanayolimwa na wakulima mbali mbali hapa nchini.