Jela miaka 20 kwa kukutwa na nyama ya twiga
8 May 2024, 11:02 pm
Hakimu wa wilaya ya Babati Victor Kimario awahukumu kwenda jela miaka 20 Paul Himid na Athumani kwa kukutwa na nyama ya twiga,kichwa na mkia wa twiga kinyume cha sheria.
Na George Agustino
Mahakama ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imewahukumu kwenda jela miaka 20 Paulo Himidi john mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa mapea kata ya magugu na Athumani Issa Misanya mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa mamire kwa kosa la uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za serikali kinyume na kifungu cha sheria namba 86.
Mawakili wa serikali Mwanaidi Chuma na wakili Getrude Kariongi pamoja na Shahidu Kajwangya ambao ni waendesha mashtaka kutoka Mamlaka ya wanyama pori Tanzania wamesema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo February 2 2024 ambapo walikutwa na nyara hizo za serikali ambazo ni kichwa kimoja cha twiga ,mkia wa twiga, ngozi pamoja na nyama vyote vikiwa na thamani ya zaidi shillingi million 50 za kitanzania.
Wakili Getrude ameiomba mahakama itoe adhabu stahiki ili iwe fundisho kwa wengine wanaojihusisha na makosa kama hayo ya ujangili kwakua twiga ni kivutio cha utalii na serikali inapata fedha za kufanya maendeleo mbalimbali ya kijamii ikiwemo kujenga shule, hospitali na miundombinu ya maji kupitia twiga