FM Manyara

Kamanda Katabazi  ashiriki swala ya kuliombea taifa Manyara

April 21, 2024, 12:31 am

Picha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara upande wa kulia pamoja na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Kamanda wa polisi mkoani Manyara Geogre Katabazi amechangia shillingi milioni moja ya ununuzi wa eneo la  jengo la msikiti na kuwaomba viongozi wa dini kuendelea kukemea vitendo viovu na kuliombea taifa.

Jeshi la polisi mkoa wa Manyara limewaomba viongozi wa dini mkoani hapa na kwingineko kuendelea kukemea vitendo viovu katika jamii ikiwemo ukatili wa kijinsia kwa watoto ili vitendo hivyo vipungue mkoani hapa .

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara  George Katabazi ameyasema hayo  aliposhiriki swala ya Ijumaa katika msikiti wa Rahma uliopo mjini Babati mkoani Manyara na kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kama jeshi la polisi kuunga mkono ununuzi wa eneo la kupanua msikiti huo.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara

Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Shekhe Mohamed Kadidi  amesema wamepokea maombi hayo na watayafanyia kazi ambapo wamefanya dua maalum ya kuliombea taifa ili Mwenyezi Mungu aliepushe na majanga yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwa ni agizo la Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakar Bin Zuberi kwa viongozi wote wa dini ya kiislam kufanya dua hiyo.

Sauti ya Shekhe mkuu wa mkoa wa Manyara