Gekul ashinda rufani
15 April 2024, 11:14 pm
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Manyara yatupilia mbali shauri la rufani yajinai dhidi ya Hashimu Ally na Pauline Gekul
Na George Agustino
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Manyara imetupilia mbali shauri la rufani yajinai namba 577 la mwaka 2024 kati ya Hashimu Ally na Pauline Philip Gekuli mbunge wa Babati mjini mkoani Manyara kutokana na pingamizi zilizotolewa na mjibu rufani ambaye ni Pauline Gekuli kupitia wakili wake Ephraim Philemon Kisanga.
Akitoa maamuzi hayo leo jaji wa mahakama hiyo Devotha Kamuzora amesema mahakama imeridhika na sababu tatu za pingamizi ya mjibu rufani na moja yapingamizi zilizotolewa na mleta rufaan Hashimu Ally ni kupeleka rufaa katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Manyara kwakua shauri namba 179 la jinai lili sajiliwa katika mahakama ya wilaya ya Babati ambalo linaendelea licha ya kuondolewa nchini ya kifungu cha 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
kwa upande wake wakili wa mkata rufani Peter Madeleka amesema hawajakubaliana na maamuzi ya mahakama kutokana na jaji kutafsiri vibaya kifungu cha sheria namba 91 kifungu kidogo cha kwanza.
Naye wakili wa mjibu rufani Ephraim Kisanga amesema wanashukuru kushinda rufani hiyo dhidi ya Hashimu Ally kwa kupeleka pingamizi zenye mashiko mbele ya mahakama na kumfanya Pauline Gekuli kuwa huru kwa mara nyingine tena mpaka watakapo pokea shauri jingine.