Wananchi Manyara watakiwa kuchukua tahadhari ya mvua
9 April 2024, 3:05 pm
Wananchi waishio mabondeni mkoani Manyara wametakiwa kuchuku tahadhari.
Na George Agustino
Wananchi mkoani Manyara wanaoishi katika maeneo ya mabonde na kwenye miteremko wametakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha kwa mwezi huu wa April na kutarajiwa kumalizika mwezi wa tano.
Wito huo umetolewa na mtaalam na mchambuzi wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) mkoa wa Manyara Rose Sinyagwa, ambaye amesema katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi wa nne mvua kubwa za masika zinatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara na kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuchukua tahadhari ili kuepuka majanga yatokanayo na mvua hizo,
Aidha amewataka wananchi kuwatumia wataalam wa kilimo ili kupata ushauri wa mazao wanayotakiwa kupanda kutokana na eneo husika walilopo ili kunufaika na mvua hizi za masika.