FM Manyara

Mkoa wa Manyara wapaa mashindano Tajwid

April 3, 2024, 5:05 pm

Picha ya shekhe wa mkoa wa Manyara akikabidhi zawadi kwa mshindi

Shekhe Kadidi aipongeza BAKWATA kwa kuuheshimisha mkoa wa Manyara

Na mwandishi wetu Hawa Rashid

Shekhe mkuu wa mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi amelishukuru baraza kuu la wa Islam Tanzania BAKWATA  kwa kuuheshimisha mkoa wa Manyara katika mashindano yakusoma Quraan tukufu kwa kisomo cha tajwihid na mshindi wa pili kutoka mkoa wa Manyara.

Shekhe Kadidi ameyasema hayo katika msikiti wa Hayatul islamia uliopo wilayani Babati mkoani Manyara baada ya kumpokea mshindi wa pili wa mashindano yakusoma Quraan tukufu tajwhid Warda Ally mwenye umri wa miaka 19 kutoka Dar es salaam alipokwenda kushiriki  mashindano hayo,ambapo amemtaka kuwa mwalimu mzuri kwa waumin wa wadini ya kiislam kwakua amejiridhisha kuwa anauwezo mkubwa wakusoma quraan tukufu.

Sauti ya shekhe wa mkoa wa Manyara

Aidha, shekhe wa mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi amemkabidhi Warda cheti cha ushiriki wamashindano hayo nazawadi mbali mbali pamoja kitabu cha dini ya kiislam ( msahafu) ili kuendelea kumjengea uwezo wakushiriki mashindano mengine.

kwaupande wake mshindi wamashindano hayo Warda  Ally amesema sababu iliyopelekea kushinda mashindano hayo ni juhudi zake za kuzingatia aliyofundishwa na maelekezo aliyopopewa namwalimu wake ambapo amewataka mabinti wakiislam kusoma madrasa nakuzingatia wanayo fundishwa

Sauti ya mshindi wa mashindano

Nae mjumbe wabaraza la mashekhe mkoa wa Manyara shekhe Hud Hud kutoka kata yakash amesema ushindi wa Warda niheshima kwa mkoa wa Manyara na lengo la mashindano hayo nikuwasadia vijana kulelewa katika mazingira ya dini nakuwaepusha kuwa majambazi katika mazingira wanayoishi.

sauti ya mjumbe wa baraza la mashekhe

Aidha, mashindano hayo yakusoma Quran tukufu kwa kisomo cha tajwihid yamefanyika jiji Dar es saam mikocheni katika ukumbi myfare ambapo washiriki walikuwa wanne kutoka mikoa mitatu ikiwepo Dar es salaam, Dodoma, Manyara na Arusha ambapo mshindi wa kwanza ametokea Dodoma nakupewa zawadi ya shilling laki sita na mshindi wapili ametoka  Manyara ambaye amepewa shilling lakitano.