Watatu wauawa akiwemo mama mjamzito Manyara
15 March 2024, 11:27 pm
Polisi Manyara inamshikilia Ahita Dahachi (42), kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi na mama mjamzito.
Na Mzidalfa Zaid
Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ahita Dahachi (42), kwa tuhuma za kuwaua watu watatu akiwemo mama yake mzazi pamoja na mama mjamzito.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara SACP. George Katabazi amesema tukio hilo limetokea Machi 13 mwaka huu katika kata ya Sirop wilayani Hanang’ mkoani Manyara. Amesema mtu huyo anadaiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili ambapo jeshi hilo linaendelea na uchuguzi wa tukio hilo.
Aidha baadhi ya mashuhuda wamesema walisikia kelele kutoka katika tukio yalipofanyika mauaji hayo baada ya kufika katika eneo hilo walimkuta mtuhumiwa huyo na kusema tukio la namna hiyo ni la kwaza katika kijiji hicho.