FM Manyara

Mtoto wa miaka 7 Babati auwawa kwa kutenganishwa kichwa, kiwiliwili

February 20, 2024, 7:14 pm

Mtoto wa miaka saba  ameuwawa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili wilayani Babati mkoani Manyara

Na Mzidalfa Zaid

Mtoto mwenye umri wa miaka saba   ambaye ni mwanafuzi wa chekechea  ameuwawa kwa kuchinjwa na mtu asiyejulikana katika kijiji cha Mapea kata ya magugu wilayani babati mkoani Manyara.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Mapea Filmon Mbogo, amekiri kutokea kwa tukio hilo katika kijiji chake nakusema baada ya kupata taarifa hizo ameliarifu jeshi la polisi ili kupata maelekezo kuhusu mwili huo.

sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Mapea Filmon Mbogo

Kwa upande wao wananchi  wa  kijiji cha Mapema wamesema mtoto huyo alikuwa anasoma katika shule ya msingi Mapea, na wakati wakitoka shule walikutana na mtu wasiomfahamu ambaye aliwadanganya  anakwenda kuwachumia mazambarau ambapo alimchukua mtoto huyo nakwenda kumchinja shambani kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.

sauti za wananchi wa kijiji cha Mapea

Aidha, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio nakusema atatolea ufafanuzi baada ya kupata taarifa kamili.