Vwawa FM Radio

Mvua yawaacha watoto watatu wenye ulemavu bila makazi

19 November 2026, 1:00 pm

Mmoja wa watoto wenye ulemavu wa miguu wa familia hiyo. Picha na Anyisile Fredy.

Mvua iliyoambatana na upepo mkali yaezua nyumba ya familia ya Peter Mwashipa, yenye watoto watatu wenye ulemavu wa kushindwa kutembea na kuzungumza.

Na Anyisile Fredy

MLANGALI

FAMILIA ya Peter Mwashipa mkazi wa kata ya Mlangali wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe yenye watoto watatu wenye ulemavu wa kushindwa kutembea na kuzungumza kwa sasa inapitia wakati mgumu baada ya Mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yao.
Akizungumza jana Novemba 18,2026 baba wa watoto hao Peter Mwashipa na Mama wa watoto hao Kisa Kyungu wamesema Janga hilo limeiacha familia yao katika hali ngumu kwani watoto wao watatu wanahitaji uangalizi wakaribu kutokana na hali zao.

Sauti ya Peter Mwashipa (Mzazi)

Mwenyekiti wa kitongoji cha Isela Selina Mwanda amesema familia hiyo kwa sasa inapita wakati Mgumu kulingana na hali yao akiomba wadau kuwashika mkono ili waweze kuwadumia watoto wao.

Sauti ya Selina Mwanda

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mlangali Mh.David Mboya ametoa wito kwa wadau wakiwemo viongozi na watu wenye moyo wa utu kujitokeza kuisaidia familia hiyo kurejesha makazi na kupata mazingira salama ya kuishi.

Hali kadhalika amesema pia wadau hao wanaweza kutoa msaada wa bima ya Afya huku akiipongeza familia hiyo kwa mshikamano wanao uonesha kwenye malezi ya watoto wao.

Sauti ya Mh. David Mboya