Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
8 November 2026, 9:59 am

Elimu ya afya ya udongo yatolewa kama silaha ya kuongeza tija ya kilimo na matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima
Na Nkopeye Mwazembe
WADAU wa sekta ya kilimo wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe wametakiwa kuimarisha huduma ya utoaji wa elimu ya afya ya udongo kwa wakulima ili kuwawezesha kutumia Mbolea kulingana na mahitaji halisi ya Udongo.
Wito huo umetolewa jana Novemba 5, 2026, na Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Solidaridad Roselaida Ngowi kwenye Jukwaa la Wadau wa Kilimo lililofanyika wilayani Mbozi.
Naye Meneja wa kituo cha utafiti wa zao la Kahawa (TacRI) kituo cha Mbimba Dismas Panglasi,amesema afya ya udongo ni moja ya nguzo muhimu katika kuongeza uzalishaji na kuboresha ubora wa kahawa
Kupitia tafiti na huduma za uchunguzi wa udongo na mimea, TaCRI inalenga kuwasaidia wakulima kupata taarifa sahihi zitakazowawezesha kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya mbolea.