Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
6 June 2025, 12:39 pm

Ni pamoja na kupata elimu ya lishe bora na afya ya watoto
Na Mwandishi wetu
Wazazi na walezi wa watoto chini ya miaka mitano kitongoji cha Isangu Mbozi mkoani Songwe wamehimizwa kufika kliniki na kuwalisha watoto chakula bora ili wakue wakiwa na afya ya mwili na akili.
Mtoa huduma ya afya ngazi ya jamii wa kitongoji hicho , Mary Mwashilindi alisema hayo alipotoa elimu ya jinsi ya kulisha watoto kwenye kliniki ya kupima kila mwezi ambayo wazazi wanakutana kituo cha godauni kupima watoto badala ya kwenda Hospitali ya Vwawa ambako ni mbali.
Mary aliwasihi wanaonyonyesha kuendelea kuwanyonyesha watoto wao huku wakizingatia masuala ya kuwalisha vyakula vya aina mbalimbali yakiwamo matunda.
Aidha Diwani wa Kata ya Hasanga Mbozi Mh.Malick Nzowa aliwapongeza wazazi waliofika kwa wingi kwenye kliniki hiyo na kwamba inafanyika hapo kwa muda na kwamba malengo ya baadaye ni huduma zote zifanyike kwenye kituo cha afya ambacho kinaendelea kujengwa Isangu.
Alitoa wito kwa wenye watoto kufika kwenye kliniki kujua maendeleo yao.
Aidha baadhi ya wanawake wameeleza mambo wanayopata kwenye kliniki hiyo. Wanawake wengine wakiwa na watoto wao wametaja yaliyojiri kwenye kliniki ya jana.