Vwawa FM Radio

Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Songwe latoa elimu

5 May 2025, 12:46 pm

Sajenti Ahobokile Lugembe (kushoto) akitoa elimu kwa wananchi wa Vwawa. Picha na John Kiango

Elimu ya wazi yatolewa kwa wananchi wa Wilaya ya Mbozi juu ya namna ya kujikinga na majanga ya moto yanapotokea.

Na John Kiango

Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Songwe limewataka wakazi wa mkoa wa Songwe kutambua mbinu za kujiokoa wakati wa majanga hususa ya moto na maji.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Songwe, FC Catherine Mgongolwa amesema lengo la utoaji wa elimu hiyo ni kuongeza ushirikiano kati ya jeshi na wananchi katika kukabiliana na majanga ya moto na kusaidia kuokoa maisha na mali

Sauti ya FC Catherine

Mmoja wa wakazi wa Vwawa Edwin Songa amezungumzia jinsi alivyopokea elimu hiyo

sauti ya mwananchi