Vwawa FM Radio

Wajasiriamali Mbozi watakiwa kuchangamkia mikopo maalumu

25 June 2026, 8:44 am

Pichani ni Vijana wajasiliamali walioshiriki kwenye kongamano la vijana kata ya Hasanga. Picha na Mkaisa Mrisho

Watakiwa Kuchangamkia Mikopo Maalumu

Na Mkaisa Mrisho

HASANGA

WAJASIRIAMALI wadogo  wilayani Mbozi mkoa wa Songwe wametakiwa kuchangamkia mikopo maalumu kwa ajili ya kundi hilo ambayo inatolewaa na Halmashauri kwa lengo la kuwaongezea mitaji yao. Ofisa maendeleo wilaya ya Mbozi Tusajigwe Mwakyembe ametoa rai hiyo juni 24, 2026 kwenye Kongamano la vijana wa kata ya Hasanga liliofanyika Godaun la Isangu.

Tusajigwe amesema mikopo hiyo ni tofauti na ile ya asilimia kumi ambayo pia hutolewa na Halmasahauri kwani mikopo huhusisha mkopaji pekee na siyo kikundi.

Sauti ya Tusajigwe Mwakyembe

Amewataka vijana wanaojihusisha na kazi ya ujasirimali mdogomdogo kutumia fursa hizo vizuri ili kukuza uchumi wao,kwani mkopaji atarejesha mkopo huo kwa riba ya asilimia 7 pekee.

Naye mshiriki kwenye kongamano hilo Ajira Mnkondya amewataka vijana kuweka utaratibu wa kushiriki makongamano yanayoanadaliwa kwenye maeneo yao ili kujua fursa zilizopo.

Sauti ya Ajira Mnkondya

Katika kongamano hilo limehudhuriwa na polisi kata wa Kata ya Hasanga Joseph Sabale ambaye ametoa wito kwa vijana kulinda amani kwani ndiyo msingi mkubwa wa Fursa kwao.

Sauti ya Joseph Sabale