Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
13 May 2026, 12:27 pm

Suala la umeme jazilizi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Na Stephano Simbeye
LONDONI: WAKAZI wa kitongoji Cha Londoni kata ya Hasanga, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wamemkumbusha diwani wa kata ya Hasanga, Mh.Malick Nzowa suala la umeme jazilizi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Mkazi wa kitongoji hicho Laki Mbalwa amesema wamepokea kiwango kidogo Cha nguzo za umeme jambo linalosababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme.
Kwa upande wa barabara Tobias Lyanda amesema barabara zimekuwa changamoto ambapo pia wakazi wapya wa maeneo hayo wanazuia barabara hizo.
Akijibu hoja hizo, diwani, Malick Nzowa amesema suala la umeme ataendelea kulifuatilia Ili kuhakikisa vitongoji ambavyo hafijafikiwa na umeme vinapata huduma hiyo.
Kuhusu Barabara Mh.Nzowa amesema ndani ya kata Hasanga zipo baadhi ya barabara ambazo zimeingizwa katika bajeti ya mwaka fedha 2026/27 unaotarajiwa kuanza Julai huku akitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kutengeneza barabara ambazo hazijasajiliwa na Serikali.