Vwawa FM Radio

Kambi ya madaktari bingwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.

21 April 2026, 9:34 am

Mkuu Wa Mkoa Wa Songwe Mhe. Jabiri Makame (wa pili kutoka kushoto). Picha na Devi Moses

Zaidi ya wagonjwa 300 wamepata matibabu siku ya kwanza

Na Devi Moses

ZAIDI ya wagonjwa 300 wamepata matibabu siku ya kwanza ya kambi ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.

Kambi hiyo imefunguliwa rasmi April 20, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Makame, ambaye amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia fursa hiyo kupata matibabu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa 1

Aidha, Mhe. Makame ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma zinazotolewa katika kipindi hiki.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa 2

Kwa upande wake, kiongozi wa madaktari bingwa katika Kambi hiyo John Meda, ameahidi kutoa huduma mchana na usiku hadi wagonjwa wote watakapohudumiwa.

Sauti ya John Meda

Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Juma Ramadhani, amesema vifaa tiba vipo vya kutosha, changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa wataalamu bingwa na bobezi kwa baadhi ya magonjwa, amewataka watumie fursa hiyo kupata matibabu.