Vwawa FM Radio

Wakulima zao la palachichi Mbozi (MAP) wameshauriwa kusajili kikundi

20 May 2026, 7:01 pm

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha wakulima wa parachichi . Picha na Stephano Simbeye

Chama cha Ushirika cha Msingi (Amcos) ambapo kuna fursa nyingi

Na Stephano Simbeye

KIKUNDI cha Wakulima wa zao la palachichi wilaya ya Mbozi (MAP) wameshauriwa kusajili kikundi hicho kuwa chama cha msingi cha u Shirika(Amcos) ili waweze kunifaika na fursa zilizopo. Mtaalamu wa kilimo cha zao hilo kutoka TAHA Ernest Mwakaleja, Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano mkuu wa kikundi hicho uliofanyika katika ukumbi wa Jekas ilembo wilayani Mbozi.

Sauti ya Ernest Mwakaleja

Amesema kutokana na kikundi hicho kuongeza idadi ya wana chama ambao idadi yao inafikia 108 inatosha kusajili ili kiwe Chama cha Ushirika cha Msingi (Amcos) ambapo kuna fursa nyingi kama vile kupata huduma za ugani, Pembejeo  na mikopo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Philbert Landa akifafanua amesema mafanikio waliyopata katika uzalishaji wa zao la palachichi yanatokana na umoja wao hivyo amewaasa wanachama kutoyumba.

Sauti ya Filbert Landa

Mmoja wa Wakulima wa palachichi Edmund Siwale ambaye siyo m wanachama wa kikundi hicho, amesema kuanzishwa Ushirika huo utakuwa na manufaa mengi kama ilivyo kwa wakulima wa mazao mengine kama kahawa. Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Afisa Kilimo Tito Njowela aliyemwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbozi amesisitiza kwamba kikundi hicho kina sifa ya kuwa Chama cha Ushirika hivyo hatua za kuelekea huko zichukuliwe

Sauti ya Tito Njowela