Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
13 May 2026, 11:51 am

umuhimu wa kuhifafhi mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Na Stephano Simbeye
CHITETE: JAMII imeaswa kuanza kulea watoto na kuwafundisha umuhimu wa kuhifafhi mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi tangu wakiwa wadogo.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa sehemu ya Uchumi na Mipango katika Halmashauri ya wilaya Momba mkoani Songwe Abel Batwel wakati akifungua kongamano la mabadiliko ya tabianchi lililoandaliwa na Shirika la SCAAP.
Amesema miaka ya nyuma mvua ilikuwa inanyesha muda mrefu tofauti na sasa ambapo mvua inachelewa kuanza na inawahi kukatika.
Mkulima kutoka kata ya Chitete David Gombela amesema mabadiliko ya tabianchi yanachangia kuwarudisha nyuma kiuchumi kutokana na hali ya hewa kutojulikana
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la SCAAP Adam Siwingwa amesema lengo la kongamano hilo ni kushirikisha jamii na mamlaka za serikali za mitaa kuhusu kuweka mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza bajeti.