Vwawa FM Radio

Mbozi wakulima wahimizwa kuhifadhi Udongo

19 September 2026, 9:15 am

Roselida Ngowi wa SOLIDARIDAD akiwaelimisha wakulima kutengeneza mboji. Pixha na Stephano Simbeye

Wakulima wahimizwa kutengeneza mboji kutokana na masalia ya mazao, ili kurejesha virutubisho na kuimarisha uzalishaji.

Na Stephano Simbeye

MBOZI

WAKULIMA wa kahawa wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe, wameshauriwa kuanza kutumia tecknolojia ya kuhifadhi udongo na yenye kuongeza virutubisho kwa kutumia masalia ya mazao.

Hayo yameelezwa na mtaalamu wa kilimo toka Shirika la SOLIDARIDAD Roselaida Ngowi wakati akifanya mafunzo na wakulima wa Amcos ya Uzalishaji Mali Ilembo(UMI) katika kata ya Hasamba.

Sauti ya Mtaalamu Roselaida Ngowi

Nao baadhi ya wakulima walioshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Modesta Mgode wameeleza kwa ufasaha jinsi walivyojifunza.

Sauti ya Modesta Mgode

Kwa upande wake mkulima mkufunzi wa Chama hicho Alinikisa Kasekwa ameeleza manufaa watakayoyapata kwa kutumia taka zitokanazo na mazao.

Sauti ya Alinikisa Kasekwa

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Edward Nzunda amelishukuru Shirika la SOLIDARIDAD kwa kuwawezesha wanachama wa Amcos yao kupata maarifa na kuwa hii si Mara ya kwanza.

Sauti ya Edward Nzunda

Uzalishaji wa mazao mbalimbali katika wilaya ya Mbozi unakabiliwa na changamoto ya kupungua kwa virutubisho kwenye udongo, hivyo kulazimu wakulima kutumia mbolea nyingi, ujio wa tecknolojia hii ukizingatiwa utawasaidia kuimarisha afya ya udongo hatimaye kuongeza uzalishaji.