Vwawa FM Radio

Vijana wa Jkt Itaka waaswa kulinda afya ya mwili na akili

13 September 2026, 11:08 am

Baadhi ya Vijana waliohitimu mafunzo ya awali Jkt Itaka wakiwa katika Gwaride. Picha na Stephano Simbeye

Vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi JKT Itaka, Mbozi, wameaswa kulinda afya ya mwili na akili ili waweze kulitumikia taifa kwa uadilifu.

Na Stephano Simbeye

MBOZI

VIJANA wanaohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kikosi cha JKT Itaka kilichopo wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe, wameaswa kuepuka vitendo vyote vitakavyoathiri afya ya Mwili na akili.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 11 mwaka 2026 na mwakilishi wa mkuu wa majeshi Brigedia Jenerali Solotina Nshushi, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo yao yaliyohusisha makundi mawili ya vijana ambayo ni kundi la vijana wa kujitolea operesheni Nishati safi na kundi la lazima (kwa mujibu wa Sheria) operesheni linda Amani.

Sauti ya Brigedia Solotina Nshushi

Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha 845 Kj Itaka Kanal Gervas Chitola amesema mafunzo ya awali ya vijana hao yalihusisha nadharia na vitendo kuwahamisha kutoka uraia kuwa kijeshi na pia wamefuzu vizuri hatua hiyo.

Sauti ya Kanali Gervas Chitola

Awali, wahitimu wa mafunzo hayo kupitia risala yao, walieleza jinsi walivyonufaika na mafunzo hayo na kuahidi kuyatumia katika maisha yao ya kila siku.

Sauti ya msoma risala Neema Simon

Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo Mhe Hamad Mbega, kabla ya kufunga mafunzo hayo, amewataka wahitimu kutumia vyema mafunzo waliyoyapata, kujiepusha na vitendo viovu na kuepuka matendo yanayoweza kutafsiriwa kuwa usaliti kwa taifa lao.

Sauti ya Mhe. Hamad Mbega (Mkuu wa (W) Mbozi