Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
1 October 2026, 12:57 pm

Tahadhari ya mvua za El Nino ambazo zimetangazwa na mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA)
Na Nkopeye Mwazembe
Wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi wametoa wito huo jana Septemba 29, 2026 wa kuhakikisha kundi hilo linakuwa salama wakati huo wa Mvua za El nino ambazo zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu.
Miongoni mwa wananchi waliotoa wito huo ni Amanyisye Mulungu mkazi wa Isangu na Clara Michael mkazi wa Vwawa wamesema kuwa jamii inapaswa kuhakikisha watu wenye ulemavu hawabaki nyuma wakati wa kuchukua tahadhari hizo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Songwe, Abel Mwakajila ameiomba jamii kushirikiana na serikali kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapatia vifaa saidizi pamoja na mahitaji muhimu.
Amesema ushirikiano kati ya Serikali, jamii na watu wenye ulemavu ni muhimu katika kuhakikisha kundi hilo linakuwa salama na linapata huduma muhimu wakati wa majanga.