Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
6 November 2026, 4:48 pm

Makazi hayo yatakuwa na huduma tofauti za kijamii kwa lengo la kuboresha ustawi wa wazee hao
Na Nicholaus Ndabila
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu, wakili Amon Mpanju amesema hayo Novemba 4,2026 wakati wa Ufunguzi wa kongamano la wazee kitaifa linalofanyika mkoani Songwe. Mpanju amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wazee wanapata huduma bora
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi,Mh.Farida Mgomi, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwenye Ufunguzi huo, amesema wazee ni nguzo muhimu katika jamii.
Baadhi ya wazee walioshiriki kongamano hilo wamesema jamii inapaswa kuthamini mchango wa wazee, huku wakieleza kuwa elimu waliyoipata itasaidia kuimarisha maadili .
Kongamano hilo limejikita katika kujadili namna wazee wanavyoweza kuwa chachu ya maadili mema katika jamii, pamoja na kutoa elimu kuhusu Sera ya Wazee inayolenga kuboresha haki, mahitaji na ustawi wao.