Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
6 November 2026, 4:16 pm

Uhaba wa nyumba za walimu kuna nyumba moja pekee kati ya 38 zinazohitajika
Na Stephano Simbeye
SHULE ya sekondari Isangu iliyopo kata ya Hasanga wilayani Mbozi mkoa wa Songwe inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu ikiwa na nyumba moja pekee kati ya 38 zinazohitajika.
Hayo yamebainishwa kwenye risala iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo mwalimu Ferida Mtafya katika mahafali ya 17 ya kidato cha nne iliyofanyika shuleni hapo Jana Novemba 5,2026.
Mwalimu Ferida amesema uongozi wa shule kwa kushirikiana na wazazi unaendelea kutatua baadhi ya changamoto ili kuwezesha wanafunzi kusoma vizuri.
Kwa upande wao wanafunzi wahitimu katika risala yao wamesema
Akizungumza katika mahafali hayo meneja wa benki ya NMB tawi la Mbozi Mumba Musa amewasihi wahitimu kwenda kutumia vizuri tecknolojia pasipo kuathiri maadili ya jamii.