Vwawa FM Radio

Mvua zawaacha wakazi wa mpanda bila makazi, msaada wafika

8 November 2026, 10:57 am

Kamati ya usalama wilaya ya Mbozi imetoa msaada kwa waathirika wa mvua Nyimbili. Picha na Anyisile Fredy

Mvua zaharibu nyumba mpanda, kamati ya ulinzi na usalama yafika na msaada kwa waathirika

Na Anyisile Fredy

KAMATI ya ulinzi na usalama wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Mh.Farida Mgomi imetoa msaada kwa wakazi wa kijiji cha Mpanda  kata Nyimbili waliothirika na Mvua iliyoharibu Nyumba zao.

Msaada huo uliotolewa Novemba 7, 2026, unajumuisha magodoro mawili na blanketi moja kwa kila kaya, pamoja na sabuni.

Sauti ya Mhe. Farida Mgomi

Naye Diwani wa Kata ya Nyimbili, Mh. Charles Kayuni, amesema msaada huo umekuwa faraja kwa waathirika na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kufuatilia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Sauti ya Diwani Mh. Charles Kayuni

Kwa upande wao, baadhi ya waathirika, akiwemo Emanuel Mwamlima na Eva Mwahoa, wamewashukuru wananchi wenzao kwa mshikamano waliouonyesha wakati wa changamoto hiyo.

Aidha, wamesema wataimarisha nyumba zao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu.

Sauti za Wananchi