Radio Jamii Kilosa

“Magufuli ameacha haya wewe na mimi tutaacha nini?”-Padri Nyanga.

27 March 2021, 4:34 am

Waamini wakatoliki Kilosa wakiwa katika ibada ya misa takatifu kumuombea Hayati Dkt Magufuli .

Waamini wa Kanisa Romani Katoliki Parokia ya Familia takatifu Kilosa Mkoani Morogoro wamefanya ibada ya misa takatifu kwa ajili ya kumuombea hayati Dakta John Pombe Magufuli katika safari yake ya mwisho ambapo machi 26 2021 mazishi yamefanyika Nyumbani kwao Chato Mkoani Geita.

Padri Richard Simon Nyaga akiongoza ibada ya misa takatifu kumuombea Dkt Magufuli katika Palokia ya Familia takatifu Kilosa

Akiwahubilia waamini katika ibada hiyo ambayo imefanyika Machi 26 2021 katika kanisa hilo Padri Richard Simon Nyanga amesema hayati Dkt John Joseph Pombe Magufuli amekufa kimwili lakini kiroho ataendelea kuishi hapa Duniani kutokana na maono yake ,utendaji kazi wake Falsafa zake za hapa kazi tuu na mambo mema aliyofanya na kuyaacha kama alama ya kukumbukwa.

Nyanga amesema kuwa Kifo Cha Hayati Dkt Magufuli kinatukumbusha sote kutafakali kwa kina na kutambiua kuwa Mungu yupo na anapaswa kuabudiwa kula wakati kwa ,kufanya toba ya kweli na kumrudia yeye kwani hakuna anaejua siku wala saa ya kufa.

Waamini wakiwa katika ibada ya misa takatifu kumuombea Hayati Dkt Magufuli

Aidha Nyanga amewataka waamini kujiuliza Magufuli amekufa ameacha hayo je mimi na wewe tutaacha nini kwa watoto , Jamii na Taifa kwa ujumla kama alama ya kukumbukwa?na kuongeza kuwa huu ni wakati sasa wa kutafakali juu ya ukuu wa Mungu hasa katika juma kuu la kwaresma linaloanza wiki ijayo Ameeleza kuwa kila mwanadamu yupo katika safari ya matumaini kuelekea mbinguni na kila mmoja anatamani kufika huko Magufuli ameumaliza mwendo hivyo kila mmoja anapaswa kujiandaa vyema na maisha mapya baada ya hapa Duniani ili aweze kufika mbinguni.

Hata hivyo Hayati Dkt John pombe Joseph Magufuli alifaliki Dunia machi 17 ,2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo machi 26 2021 amepumzishwa katika Nyumba yake ya milele Wilayani Chato Mkoani Geita.