Radio Jamii Kilosa

Jamii imetakiwa kula Mlo kamili kuimarisha Kinga ya Mwili-Kilosa

21 January 2021, 1:44 pm

Mratibu wa Shughuli za Wahudumu kutoka Mradi wa Lishe Endelevu Wilayani Kilosa Bwana Revocatus Mussa akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Radio jamii Kilosa Christiani Kilewa kushoto kwenye kipindi cha Mambo mseto.

Wito umetolewa kwa jamii kula Mlo kamili kwa kuzingatia makundi matano ya Chakula ili kuimarisha Kinga ya Mwili Isishambuliwe na magonjwa.

Wito huo umetolewa januari 21, 2021 na Mratibu wa Shughili za Wahudumu kutoka Mradi wa Lishe endelevu Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Bwana Revocatus Mussa alipokuwa kwenye mahojiano maalumu katika kipindi Cha Mambo Mseto Kinachorushwa na Radio jamii kilosa juu ya Umuhimu wa Makundi matano ya chakula katika mwili.

Amesema kuwa kuna umuhimu wa kula Mlo kamili ambao unamchanganyiko wa Makundi yote matano ya chakula ambayo ni Wanga, Protini,Mafuta, Matunda na Mbogamboga pamoja na Vitamini kwani unasaidia Kuimalisha Kinga ya mwili kuujenga na kuupa Nguvu ikiwa ni pamoja na kuepuesha mwili usishambuliwe kirahisi na magonjwa nyemelezi.

Bw Mussa amesema kuwa Mwili unapokosa vyakula vya jamii ya Mikunde Nafaka na Mizizi, Nyama,Mafuta ,Matunda na Mbogamboga pamoja na Vitamini kutapelekea mwili kukosa virutubisho ambapo utapoteza muonekano halisi wa ngozi wakati mwinge midomo kuchanika na afya kudhohofika.