Radio Fadhila
Radio Fadhila
26 August 2025, 7:53 PM

“Tukichanja mbwa wetu, siku akikung’ata kutakuwa na madhara ya kawaida, tuhakikishe mbwa wanachanjwa ili kuepuka ugonjwa hatari wa kichaa cha mbwa“
Na Neema Nandonde
Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Rachel Kassanda amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuwapa chanjo wanyama wanaofugwa, ili kuepuka magonjwa yanayosababishwa na wanyama hao ikiwemo kichaa cha mbwa.
Ameyasema hayo Agosti 26, 2025 alipokuwa akizungumza katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya jamii kwa robo ya nne ya mwaka 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya Masasi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Alphaxad Etanga, amewasisitiza wajumbe wa kamati ya lishe wilayani humo kuhakikisha kuwa wanaendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora, huku akisisitiza kuwa kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni ni lazima.
Aidha amewaomba viongozi wa dini kufikisha ujumbe kwa waumini wao, kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto ili kupata chanjo ya ugonjwa wa polio.