Radio Fadhila

Jumuiya ya wazazi Masasi wakutana na kupewa nasaha

13 August 2024, 11:31 AM

Kikao cha utendaji Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Masasi wamekutana katika ofisi za chama hicho Wilayani Masasi.

Akizungumza katika Kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mtwara NDG.JULIUS MSELECHE KAONDO ametoa nasaa kwa viongozi wa Jumuiya hio kuendelea kukitumikia chama kwa weledi kwani katika uongozi wa chama kujitolea ni kwingi zaidi kuliko mafao.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Masasi Ndg PIUS AMULI amesema wao kama wilaya jukumu lao kubwa ni Elimu Malezi na Mazingira.