Radio Fadhila

RC Mtwara azungumza katika jukwaa la ushirika 2024

21 June 2024, 9:18 PM

Mhe Kanali Patrick Sawala alizungumza

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe: Kanali Patrick Kenan Sawala amezungumza na viongozi wa vyama vya ushirika katika jukwaa la maendeleo ya ushirika yaliyofanyika 20/06/2024 katika ukumbi wa Police mess Mtwara.

Lengo la jukwaa hilo ni kutanga uzaushirika na kaulimbiu ni “USHIRIKA HUJENGA KESHO ILIYOBORA KWA WOTE”

Mhe:Sawala aliwaomba viongozi wa AMCOS waongeze uzalishaji wa mazao Kwa kugawa pembejeo,kutoe elimu Kwa wakulima na kishauri wakulima juu wa kulima mazao zaidi ya moja ya chakula na biashara.

Sambamba na hayo mhe: Sawala amewataka viongozi kufanya kazi Kwa maslahi ya taasisi,halmashauri,wilaya,mkoa na Taifa Kwa ujumla.

Lakini pia aliwapongeza viongozi wa vyama vya ushirika ( TANECU NA MAMCU) Kwa kurudisha hisani Kwa jamii pamoja na kuajiri maafisa ugani ili kiwa karibu na wakulima .

Lakini pia aliwataka viongozi kuwa walinzi wa mazao ili yasitoke kweny halmashauri zao.