Radio Fadhila

Viongozi wa vyama vya msingi wapigwa msasa

22 May 2024, 1:34 PM

Wajumbe wapya wa bodi, mameneja, wajumbe wawakilishi pamoja na makarani wapya wa vyama vya msingi wakipatiwa mafunzo na kujengewa uwezo katika kazi na kukumbushwa majukumu yao.

Na Lilian Martin

Pamoja na kukumbusha juu ya majukumu yao katika kazi walipata nafasi ya kufundishwa namna ya matumizi ya mizani mipya ya kisasa.

Kwa upande wake katibu wa kamati ya elimu ya ushirika mkoani Mtwara Paulo Anania amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi wampya na kuwakumbusha majukumu katika vyama vyao na kutunza kumbukumbu za kifedha na umuhimu wa kufanya ukaguzi kama wasimamizi.