Mufindi FM
Mufindi FM
6 March 2026, 11:00

Viongozi wa taasisi ya Nafaka Kilimo wanaotekeleza mradi wa Farm to Market Alliance (FtMA) unaofadhiliwa na shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) katika picha ya pamoja na washiriki wa mradi huo ( viongozi wa wakulima, watoa huduma za kilimo, wafanya biashara, vyama vya ushirika) na viongozi wa serikali katika tathmini ya mwaka mmoja wa mradi. Picha na Jackson Machowa.
Mradi huo wa FtMA umekuwa msaada mkubwa wa wakulima kuanzia shambani hadi sokoni, ikiwa ni pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto zilizopo kwenye mnyololo huo wa thamani katika kilimo.
Na Jackson Machowa
Watoa huduma za Kilimo zaidi ya 300 wanaoshirikiana na mradi wa FtMA unaotekelezwa na shirika la Nafaka Kilimo wametajwa kuwa chachu ya maendeleo ya wakulima kwa kurahisisha upatikanaji wa elimu na zana za kilimo bora kwa wakulima wa mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya.
Katika kikao cha tathimini kilichofanyika mjini Makambako na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa Kilimo, mradi wa FtMA umeeleza kupatikana kwa shilingi Bilioni 29 na kuwanufaisha zaidi ya wakulima elfu 54 kutoka katika maeneo ya mradi huo kwa mwaka 2025-2026, kama anavyobainisha Godson Kakete.
Bi Esta Mkula ni miongoni mwa wanufaika wa mradi wa FtMA na ni mshiriki wa kikao washiriki wa kikao ameiambia Mufindi redio, jinsi mradi huo ulivyobadilisha maisha yake na jamii yake.
Aidha Bi. Mkuta amewasihi wanaume kuhudhuria vikao na mikutano ya elimu za kilimo bora kila inapoitishwa badala ya kuacha jukumu hilo kwa wanawake pekee hali inayoleta migongano ya kiutekelezaji.
Sauti Bi. Mkuta
Kwa upande wake mratibu wa mradi Bwana Mosses Logan ameeleza malengo ya kufanyika kwa kikao hicho tathimini ili kujua jinsi ambavyo malengo ya mradi yamefikiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Sauti Mratibu wa mradi FtMA
Awali akifungua kikao hicho cha Tathimini Afisa kilimo Mkoa wa Njombe Bw. Joel Wilson amesema kazi za mradi huo zinaakisi mipango ya serikali kuifanya sekta kilimo iweze kukua kwa asilimia kumi ifikapo mwaka 2030 huku akiomba uendelevu wa mradi huo ili uendelee kusaidiana na serikali katika kustawisha jamii kiuchumi kupitia kilimo.
Sauti Joel Wilson

Pichani ni Mgeni rasmi ambaye ni Afisa kilimo mkoa wa Njombe ndg. Joel Wilson katika kikao cha tathmini kilichofanyika Majambazi mkoani Njombe. Picha na Jackson machowa.
Ikumbukwe kuwa mradi wa Farm to Market Allience (FtMA) unaofadhiliwa na shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) kupitia shirika la Nafaka Kilimo unatarajia kumaliza muda wake wa mkataba Machi 31 mwaka huu huku ukiacha alama isiyofutika kwa wakulima wa halmashauri za Wangingombe, Njombe, Mufindi,Iringa, Kilolo, Mbeya na Mbarali.