Mufindi FM

UWT Mufindi yaadhimisha miaka 49 ya CCM kwa matendo ya huruma

3 February 2026, 11:50

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi. Marcelina Mkini akimkabidhi msaada wa sabuni na Mafuta mmojawapo wa wakina mama aliyejifungua mtoto katika hodi ya wazazi iliyopo katika Hospitali ya Mji Mafinga. Picha na Isaack Nyigo.

Ndugu zangu viongozi turudi katika miongozo ya chama inavyotuongozo ikiwemo kuvaa sare za chama, kuitisha vikao na mikutano Bi. Mkini

Na Marko Msafiri.

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Mufindi, imewataka viongozi wa jumuiya hiyo kurudi katika kanuni za chama zinazowaongoza wanachama katika shughuli mbalimbali za kichama ikiwemo kuitisha mikutano na vikao.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Marcelina Mkini, katika maadhimisho wa miaka 49 tangu kuasisiwa kwa chama hicho cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika kiwilaya katika uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga.

Sauti Bi. Mkini wito.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na matendo ya huruma katika Hospitali ya Mji Mafinga kwa jumuiya hiyo ya umoja wa wanawake kutembelea hodi ya wazazi na kutoa msaada.

Sauti Bi. Mkini matendo ya huruma.

Baada ya kukabidhi msaada huo, Elizabethi Kilenyi ambaye ni miongoni mwa wanufaika, ameipongeza jumuiya hiyo na kuwataka waendelee na moyo huo wa majitoleo.

Sauti Elizabethi.

Bi. Rehema Mbedule ambaye ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya na mshiriki katika maadhimisho hayo, amesema kama wanawake wakihamasika, watazingatia malezi na kuwaepusha vijana wasiingie katika uvunjifu wa amani.

Pichani ni Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya UWT wilaya ya Mufindi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi misaada katika Hospitali ya Mji Mafinga. Picha na Isaack Nyigo.

Maadhimisho hayo ya miaka 49 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yamebeba ujumbe usemao “Umoja na Amani kwa maendeleo ya Taifa Letu”.