Mufindi FM

RC Kheri aelekeza DED Mufindi kuwasimamia watumishi wake

16 January 2026, 15:51

Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James akipokea maelezo kutoka kwa Mhandisi wa wilaya ya Mufindi ndg. Said Kachenje kuhusu ujenzi wa madarasa katika shule mpya ya awali msingi na sekondari Mufindi katika ziara aliyoifanya wilayani humo.Picha na Isaack Nyigo.

Huwezi kufanyia kazi ya ujenzi ukiwa ofisini ” RC Kheri

Na Marko Msafiri

Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Ndg. Mashaka Mfaume kuwasimamia watumishi hasa katika maeneo matatu ikiwemo eneo la ugavi na manunuzi.

Eneo lingine ni ofisi ya uhandisi na wasimamizi wa eneo mama la mradi unaotekelezwa ili kuepusha kuzorota kwa ujenzi wa miradi endapo eneo moja kati ya hayo likishindwa kuwajibika.

RC Kheri ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali katika sekta ya elimu na afya ambapo amesisitiza kuhusu ushirikiano ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili ianze kuwanufaisha wananchi.

SAUTI RC. Kheri maagizo

Akiwa katika shule mpya ya awali, msingi na sekondari Ngwazi. Mhe Kheri amechukizwa baada ya kukuta mradi wa darasa na vyoo umesimama kutokana na ukosefu wa vifaa hasa vigae (malumalu) uliosababishwa na kutokuwajika kwa ofisi ya manunuzi na kuagiza kuwa ujenzi huo uanze mara moja.

Sauti RC. Kheri

Akijibu kuhusu kuchelewa kwa mradi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo. Ndg Mashaka Mfaume amesema kuzorota kwa mradi huo umechangiwa na aliyekuwa afisa manunuzi aliyehamishiwa wilayani hapo, kutoka wilaya ya Kilolo kushindwa kuendana na kasi ya ujenzi.

Sauti DED Mufindi

Awali wakisoma taarifa ya ujenzi akiwemo mkuu wa shule mpya ya awali, msingi na sekondari Ngwazi Mwl. Roida amesema mradi huo ulipaswa kukamilika mwezi Novemba mwaka 2025 lakini walishindwa kukamilisha kutokana na kukosa wazabuni jambo lililofanya kutangaza zabuni mara kwa mara.

Sauti Mkuu wa shule Mwl. Roida

Pichani ni kituo cha afya cha kata ya Makungu alichotembelea Mhe. Kheri na kukikagua wakati wa ziara yake ya siku mbili wilayani humo.

Mhe. Kheri ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya awali, msingi na sekondari Ngwazi, kukagua madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Kilongo na kukagua ujenzi wa kituo cha afya kata ya Makungu.