Mufindi FM

Mufindi DC yapewa maagizo mapya, Baraza la Madiwani likivunjwa

21 June 2025, 22:19

Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba akiwa katika kikao cha kuvunjwa kwa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Mufindi lililofanyika jana Juni 20, 2025. Picha na Mwanaidi Ngatala.

kuvunjwa kwa Mabaraza ya madiwani nchini ni miongoni mwa hatua katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, unaohusisha kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Na Kefa Sika

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Mufindi limevunjwa Jana June 20, 2025 ikiwa limehudumu tangu mwaka 2020_2025.

Akizungumza kwenye mkutano wa baraza hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri Itulavanu, Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ameiagiza halmshauri hiyo kukusanya Billioni 2 hadi kufikia mwishoni mwa mwezi June 2025.

Aidha Mhe. Serukamba ameisisitizia halmashauri hiyo kuunda timu ya kufuatilia madeni, ambayo watu wanadaiwa kwenye vyanzo vya mapato vya wilaya.

Mhe. Serukamba RC Iringa

Awali aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina amewapongeza madiwani hao kwa kazi waliyoifanya kwa miaka yote na kuleta maendeleo kwenye wilaya ya Mufindi.

Sauti Mhe Mgina.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi ndg. Mashaka Mfaume ameahidi kutekeleza maagizo yote kwa muda muafaka.

Baada ya baraza hilo la madiwani kuvunjwa , Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo anakaimu nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri na ana wajibu wa kuunda kamati ya kutelekeza majukumu ikiwemo kufuatilia miradi ya maendeleo.