Mufindi FM

Kilimo Masoko yaja na mkakati masoko

26 May 2025, 13:11

Wadau wa mnyororo wa thamani katika kilimo wakipata mafunzo ya kuwajengea uwezo katika ukumbi wa Valentine uliopo mkoani Iringa (Picha na Marko Msafiri)

Mafunzo hayo ni ya kuwainua wakulima kutawala katika soko la dunia kupitia uwepo wa mazingira wezeshi.

Na Marko Msafiri

Taasisi ya Nafaka Kilimo kupitia mradi wa Kilimo Masoko (FtMA) Kwa imewakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya pembejeo kwa lengo la kuondoa changamoto katika musimu wa kilimo ikiwemo udhibiti madhubuti wa mbolea na mbegu sambamba na kuangalia fursa katika sekta hiyo.

Akizungumza katika Kikao hicho, Mratibu wa mradi huo wa Kilimo Masoko Bw. Mosses Logani amesema matarajio ya mradi huo kwa wakulima ni kuongeza thamani ya mazao (kilimo biashara), usalama wa chakula na kufahamu asili ya ardhi katika eneo husika na mahitaji yake katika matumizi ya pembejeo ikiweo mbegu na mbolea.

Aidha Bw. Logani amesema mradi unawatumia mawakala wa pembejeo na kwamba matarajio ni kuwa na watoa Huduma 500 Ili kumfaidia mkulima pale anapohitaji msaada ukilinganisha na watoa huduma 200 waliopo sasa katika ukanda wa nyanda za juu kusini.

Sauti Logani

Kwa upande wake Lauret John ambaye ni Bwana shamba masoko wa Kampuni ya Yara Tanzania Limited Mkoa wa Iringa amesema kuwa wamesimama imara dhidi ya wadanganyifu katika pembejeo na kuhakikisha kuwa mkulima ananufaika zaidi na pembejeo zinazotolewa.

sauti John

Nae Chris Simike kutoka Kampuni ya Viuatilifu ya Bytter Crop amesema kuwa mafunzo hayo yataongeza thamani kwa wakulima kwani elimu hiyo ni msingi mkubwa katika kilimo.

Sauti Chris