Kalinga awashika mkono Excell malezi ya watoto
22 November 2024, 15:09
MUFINDI
Na Kefa Sika
Mdau wa maendeleo wilayani Mufindi ambaye ni Meneja wa mawasiliano na masoko wa wakala wa Majengo Tanzania Nd. Fredric Victory Kalinga amechangia zaidi ya shilling laki 5 za kitanzania kwenye kituo cha malezi na elimu ya watoto cha Excell (Excell Daycare and Nusury School) kilichopo kijiji cha kidete kata ya Mdabulo wilayani Mufindi.
Akizungumza kwenye mahafali ya pili ya kituo hicho Ndugu Fredrick Kalinga amesema kuwa changamoto zilizonyingi shuleni hapo amezitatua ikiwemo ile ya ukosefu wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa kituo hicho.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la maendeleo vijijini (Rular Development Organization) RDO Fidelis Filipatali ameahidi kuendelea kushirikiana na wamiliki wa kituo hicho ili kutoa elimu kwa watoto wa maeneo hayo.
Naye mmiliki wa kituo hicho cha Excell Bw. Isaya Juliano Kalinga amemshukuru Ndugu Fredric lkwa ujio wake kwani amesaidia kutatua baadhi ya changamoto kituoni hapo.
Awali baadhi ya wazazi wa wanafunzi waliohitimu wamesema kuwa vituo hivyo vina mchango mkubwa kwa maendeleo ya wanafunzi kielimu.
Mahafali iliyofanyika siku ya jana ni mahafali ya pili huku wanafunzi 20 wamehitimu elimu hiyo ya awali kwenye kituo hicho cha excel.