Mufindi DC yapewa kongole ujenzi Mpangatazara Sec
24 October 2024, 18:53
Shule ya sekondari Mpangatazara itawasaidia wakazi wa kata hiyo kuondokana na adha ya kutembea umbali wa 40 Hadi shule ya sekondari Mdabulo kupata elimu.
Na Fatuma Hamis
Mufindi
Mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba, ameridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Mpangatazara na ameipongeza serikali ya awamu ya 6 kwa kuwa umeme pia umefika katika kijiji hicho ambacho hakina wakazi wengi.
Serukamba ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi wilayani Mufindi katika kijiji cha Mpangatazara, na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za elimu, maji, barabara na umeme.
Nao baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo, wamesema kuwa kabala ya shule hiyo kuwepo walikuwa wanatembea umbali mrefu takribani kilomita 40 kufika shule ya sekondari mdabulo.
Baadhi ya wazazi na walezi kijijini hapo, wanaishukuru serikali kwa kuwajengea shule hiyo karibu na makazi yao, kwani walikuwa wanateseka kuwapeleka watoto wao shule ya mbali jambo ambalo liliwalazimu, baadhi ya wanafunzi kuishi kwenye kota za wafanyakazi wa serikali.
Ujenzi wa shule ya sekondari Mpangatazara utagharimu kiasi cha shilingi milioni 583 hadi kukamilika kwake.
MWISHO