Mufindi FM

Ulaji nyama ya mbuzi hatari kwa afya-Utafiti

3 September 2024, 09:33

Mwonekano wa Nyama ya mbuzi

Vinasaba vya nyama ya mbuzi vinatajwa kuwa mojawapo ya kichocheo cha ugonjwa wa maumivu ya magoti.

Na Attu Lufyagile

MUFINDI

Wananchi na wakazi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wameshauriwa kupunguza matumizi ya nyama ya mbuzi kwani husababisha ugonjwa wa mifupa hususani kwenye magoti.

Dkt. Albert Mdemu wa kituo cha afya DRL Kilichopo Kinyanambo anaeleza jinsi ambavyo ulaji wa nyama ya mbuzi kupita kiasi huathiri uimara wa mifupa.

Sauti ya Dkt Albert Mdemu

Katika kuliangazia suala hili kinagaubaga kufahamu je, watumiaji ama wananchi wana uelewa wa kutosha juu ya athari zinazoweza kuwapata?

Sauti za wananchi kuhusu nyama ya mbuzi

Kutokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema matumizi ya nyama nyekundu (nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo) kupita kiasi ni hatari kwa afya ya binadamu kwani husababisha magonjwa kama ya mifupa, kisukari pamoja na saratani, hivyo watu wapunguze matumizi ya nyama nyekundu na hata zilizosindikwa.