Mufindi FM

Waziri Mkuu Majaliwa aweka jiwe la msingi ujenzi shule ya sekondari Iramba wilayani Mufindi

9 July 2024, 08:02

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa (kulia pichani)akiweka jiwe la msingi shule ya sekondari ya wasichana Iramba wilayani Mufindi.Picha na Christogon Ngoloki

Na Bestina Nyangaro

Mufindi

Leo Julai 7 2024, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amekagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa darasa la mfano shule ya sekondari Iramba iliyopo kata ya Itandula halmashauri ya wilaya ya Mufindi.

Sauti ya Waziri Mkuu Majaliwa

Kulingana na taarifa iliyosomwa na Afisa Elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Mufindi Daniel Mapilya, .Ujenzi wa Shule hiyo unategemewa kugharimu kiasi cha Bilioni 1.78 mpaka kukamilika kwake.

Sauti ya Daniel Mapilya

Kwasasa shule hiyo ina jumla ya madarasa 8, Ofisi 4 na bweni lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 lipo katika hatua ya kuwekwa marumaru.