FM Manyara

Wafugaji Simanjiro  waaswa kupeleka mabinti shule  

7 October 2024, 9:15 pm

Wadau wa elimu kutoka shirika la Kinnapa, wafugaji kutoka wilayani humo wamesema wame elimika kutokana na elimu waliyoipata mara kwa mara  na wameamua kuwapeleka watoto wa kike shule na hasa  waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo

Na Diana Dionis

Jamii ya  wafugaji wilayani Simanjiro mkoani Manyara imetakiwa kuwarejesha wananafunzi walioacha  masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba za  utotoni

Wakizungumza na waandishi wa habari katika kikao kazi cha wadau wa elimu kutoka shirika la kinnapa, wafugaji kutoka wilayani humo wamesema wame elimika kutokana na elimu waliyoipata mara kwa mara  na wameamua kuwapeleka watoto wa kike shule na hasa  waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo.

sauti za wadau wa elimu kutoka shirika la kinnapa

Kwa upande wao wadau wa elimu kutoka shirika la kinnapa Paulina Ngurumwa na Onike Laizer wamesema wamepata mafanikio makubwa  baada ya kumrejesha mtoto wa kike shule hasa walioacha  masomo kwa sababu mbalimbali.

sauti za wadau wa elimu kutoka shirika la kinnapa Paulina Ngurumwa na Onike Laizer

Aidha baadhi ya maafisa ustawi kutoka mkoa wa Manyara wamesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuwarejesha watoto wa kike shule ambao wamefanyiwa ukatili nakushindwa kuendelea na masomo yao.

sauti ya maafisa ustawi kutoka mkoa wa Manyara