FM Manyara

Wananchi  acheni kuwaficha wahalifu

20 March 2024, 5:27 pm

Picha ya mkuu wa kituo cha polisi Babati (kulia) akitoa elimu katika kituo cha Fm Manyara

Polisi Manyara yawataka wananchi  kuripoti matukio ya kihalifu katika mitaa yao.

Na George Agustine

Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa  katika kituo cha  polisi  kutokana na watu wanaofanya matukio ya kihalifu katika mitaa yao ili wachukuliwe  hatua za kisheria na kukomesha matukio hayo.

Akizungumza na Fm Manyara katika kipindi cha Mseto wa Leo mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Babati Amiri Mlemba,amesema wananchi wanapaswa kuwaripoti wahalifu waliopo majumbani badala ya kuwahifadhi na kuacha vitendo hivyo kuendelea ambapo amesema jeshi la ulinzi shirikishi kwa kusaidiana na jeshi la polisi wamefanikiwa kuwakamata wahalifu  nyakati za usiku.

sauti ya mkuu wa kituo cha polisi Babati OCS Amir Mlemba

Aidha Mlemba amewataka waendesha pikipiki maarufu  bodaboda kuwa waangalifu hasa nyakati  za usiku kwa kutoa taarifa katika kituo cha polisi kabla hawajaanza safari yakuwapeleka abiria.

 kwa upande wake mratibu wa dawati la jinsia wilaya ya Babati Koplo Leokadia Mmanya, amesema ili kudhibiti vitendo vya uharifu mzazi anapaswa kumlea mtoto kwa maadili ili anapokua asijiingize kwenye makundi ya kiuharifu.

sauti ya mratibu wa dawati la jinsia wilaya ya Babati Koplo Leokadia Mmanya

.