FM Manyara

Wananchi wa kata ya Sarame walazimika kunywa maji machafu

7 December 2023, 6:30 am

Wananchi wa kata ya Sarame wilayani Babati mkoani Manyara wanalazimika kunywa maji machafu kutokana na ukosefu wa maji safi na salama katika kata yao. Picha na Upendo Yohana

Na Muzidalifa Zaid.

Wananchi wa kata ya Sarame  wilayani Babati mkoani Manyara, wameiomba serikali kutatua changamoto ya maji ambayo  limedumu kwa muda mrefu katika kijiji hicho na kupelekea kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.

Wananchi hao wamesema kutokana na kukosa huduma ya maji safi na  salama wanalazimika kutumia maji ya mto kwa matumizi ya kunywa na kupikia pamoja na shughuli nyingine hali ambayo huenda ikawasababishia kupata magonjwa ya mlipuko.

Sauti ya wananchi wa Sarame

kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Sarame Joseph Jura, amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa taarifa hiyo kwa viongozi wa ngazi za juu na tatizo hilo limekuwa likishindwa kutatuliwa, lakini wameishukuru mamlaka ya maji na usafi wa mazingira babati(Bawasa) kwa kufika katika kijiji hicho.

Sauti ya mwenyekiti wa Barame Joseph Emanuel Bura

Aidha, kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bawasa Rashid Charahani, ameelezea sababu ambazo zimekuwa zikipelekea kuchelewa kwa huduma ya maju katika kijiji hicho, na kuwataka wananchi wa kata hiyo kuwa na subira kwakua  Serikali  imweka mpango wa kufikisha huduma hiyo na imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji hicho.

Sauti ya Mkurugenzi wa Bawasa Rashid Charahani