Mita za maji kuhakikiwa Manyara
21 August 2024, 5:49 pm
Wakala wa vipimo mkoa wa Manyara wanatarajia kuanza msako wa kukagua mita za maji ili kubaini kama zinafanya kazi vizuri.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa kwenye ofisi ya wakala wa vipimo ili zihakikiwe kama ziko sahihi wanapobaini bili ya maji haiedani na matumizi ya maji wanayoyatumia.
Meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Manyara Dennis Misango amesema kwa sasa wanaendelea na msako wa kukagua na kuhakiki mita hizo majumbani ili kubaini mita ambazo zinatoa majibu ambayo sio sahihi.
Amewataka wananchi kufahamu namna ya kusoma unit za maji ili kujua kama matumizi yao yanaenda na bili inayotolewa na mamlaka husika huku akiitaka mamlaka ya maji kuhakikisha wanasoma vizuri uniti zinazoonyesha kwenye mita hizo.